TAMTHILIA YA WALANG HANGGAN YAZIDI KUKONGA NYOYO ZA WATAZAMAJI WA STAR TV.
![]() |
Katerina, Nathan, Johan, Thomas na Daniel |
Baada ya baba yake Katerina kufariki ghafla, sasa Thomasi “mwanae”
anajimilikisha kampuni ya baba yake kinyume na mirathi ya baba yake, huku
akimfanyia unyama Daniel.
Thomas anagundua kuwa Daniel na mdogo wake Katerina
wanauhusiano wa kimapenzi, hivyo anatekwa na wivu na kuamua kumsingizia Daniel
kuwa ameiba pesa. Thomas anaamua kumpa adhabu ya kumfunga kamba mikono na kumburuza katika shamba la baba yake.
Lakini wakati Thomas akimfanyia unyama huo Daniel, Emily
anaye sadikika kuwa huenda akawa ni mama yake alishuhudia kwa mbali mkasa huo,
kitu kilicho mkwaza sana na kumuamulu
mfanyakazi wake kumfuatilia Thomas na kubaini chanzo.
Thomas naamua kuchoma sehemu ya nyumba na kumsingizia
Daniel, ili kwamba iwe rahisi kumuhamisha Katerina pale ili akae mbali na
Daniel. Thomas anampigia sana debe Nathan awe mpenzi wa mdogo wake Katerina,
sababu iliyomfanya amuhamishie Katerina kwao Nathan ili baadae familia ya
Nathan iweze kumsaidia kifedha.
Emily anazidi kumtumia Johane binti yake Marco ili kupata
upenyo mzuri wa kulipiza kisasi katika familia hiyo. Emily ambaye sasa maisha
yake ni mazuri kifedha anaingiwa na huruma mara kwa mara akikumbuka kitendo cha
Thomas kumburuza Daniel na farasi, hivyo sasa anaanza kumfuatilia Daniel kujua
mengi japokuwa ameambiwa kuwa Daniel ni mototo wa kambo.
Siri nzito yapangwa kufichuliwa na bibi yake Daniel, huku
Emily akijipanga kulipiza kisasi kwa familia ya Marco.
Je nini kitaendelea? Karibu tena
kwa dondoo nyingine za tamthilia hii
hapa hapa.