Asili Yetu © All rights reserved
Kazi hizi uzionazo hapa ni juhudi, utaalamuna ubunifu wa hali ya juu ufanywao na akinamama hawa ambao pia ni nguzo katika familia zao. Huu ni utamaduni halisi wa kitanzania ambao ndio unaotufanya tutembee vifua mbele tuwapo katika mataifa mengine duniani.
Eneo hili lililoko mjini Arusha ni maarufu kwa vitu mbali mbali vya asili ambavyo wageni na wenyeji huja kununua.
Kama unavyoona hapa ni mbele ya eneo maalum la kuuzia vyombo vya asili mjini Arusha.
Hivi ni viatu ambavyo hutengenezwa kwa kutumia matairi ya gari yaliyokwisha kutumika.Viatu hivi ni maarufu kama "kata mbuga" japokuwa vinamajina mengi sana kulingana na sehemu zitumikazo.
Hizi ni picha zilizochorwa kwa mkono, lakini pia kuna viatu vya wazi vya asili ambavyo havipitwi na wakati.Hiatu hivi hutengenezwa kwa ngozi na kutiwa nakshi ya shanga zenye rangi mbali mbali.