Asili Yetu © All rights reserved
Goodlight Lugamalila ambaye ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Piki piki mkoani Arusha (UWAPA) akizungumza katika kikao.
Goodlight Lugamalila ambaye ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Piki piki mkoani Arusha (UWAPA) akizungumza katika kikao.
Mnamo majira ya saa nne za asubuhi nilikutana na maelfu ya piki piki zikiwa zimeegeshwa katika eneo la Silent Sakina mjini Arusha, ambapo chanzo kinaeleza kuwa ulikuwa ni mgomo wa waendesha piki piki ulioko chini ya uongozi wao wa "UWAPA" -Umoja wa Waendesha Piki piki Arusha.
Waendesha pikipiki alimaarufu boda boda mkoani Arusha leo wamegoma kwa muda usiopungua masaa sita wakipinga ongezeko la tozo ya halmashauri kulipa shilingi 500 kwa ajili ya ushuru wa magesho .
Wakizungumza kwa jaziba na kaimu kamanda wa polisi mkoa arusha wambura walisema kuwa wamepat atangazo linalowataka kulipa ushuru wa shilingi 500 kwa maegesho kwa kwasiku hali ambayo wamesema hawakubaliani nayo kutokana na kutokuwa na fedha za kulipa ushuru huo ambapo walisema kuwa watakuwa wanaumizwa.
Akiongea kwa niaba ya wenzake mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki mkoa wa Arusha Godlight Rungamulila alisema kuwa fedha hiyo la maegesho ni kubwa sana kwa wao waendesha pikipiki kwani ukipiga esabu kwa mwaka mzima inakuwa nyingi sana na ukichanganya na ushuru ambao wanalipa pamoja na Trl wanakuwa wanawaumiza sana waendesha pikipiki na pia alibainisha kuwa kinachowaumiza ni kwamba bei hiyo imepandishwa pasipo kushirikishwa wakati wao ndi wahusika .
“unajua serekali ilitutolea bei ya maegesho kwa waendesha pikipiki ambapo tulikuwa tunalipa shilingi 35000kwa mwaka sasa wanavyo tuambia tulipe shilingi 500 kwa siku si wanatukomoa kwani fedha hizo ni nyingi sana na hata ukipiga hesabu inakuja mara nne ya ile serekali ambayo imetufutia sasa sibora wangeacha ile kuliko kutuambia tulipe hela hii kwa siku”alisema mwenyekiti
Aidha mgogoro huo uliendelea hadi pale mkuu wa wilaya ya arusha John Mongela alipokuja na kutatua swala hilo ambapo aliwataka warudi katika sehemu zao za kazi na kusema kuwa wao wenyewe kama serekali hawajui swala hili na wala mkurugenzi hajui hivyo tangazo hilo ni batili.
Alisema kuwa wao kama serekali ya mkoa na wilaya wameanza kulishulikia swala hili na hadi kufikia sasa wameshamjua aliyetoa tangazo hilo na wapo katika harakati za kumchukulia hatua kali na kuwahaidi waendesha pikipiki hao kuwa ndani ya siku mbili watakuwa wameshachukuliwa hatua za kisheria..
“kiukweli mimi nilikuwa sijui wala mkuu wa mkoa na mkurugenzi na hatuwezi kupandisha bei ya maegesho pasipo kuwashirikisha nyie sisi tutawashirikisha na tutahakikisha tunakuliana ndo tufanye hivi la kini hatuwezi kukurupuka na kujichukulia sheria mkononi sisi tunafanya kazi kwa kufuata utaratibu na kanuni lakini napenda kuwaambia kuwa swala hili lililkuwepo katika mazungumzo na muafaka bado na kwanza bado sana hivyo mtu huyu aliotoa tangazo hili ni muongo sio mkweli na tangazo hili ni batili rudini vijiweni kwenu mkafanye kazi mtu yeyote asiwachaji ushuru’alisema Mongela.
Aliwataka kufuata sheria za barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinatokea mara kwa mara na pia aliwasihi kutofanya fujo ambazo zisizokuwa na mahana bali kufikiria kabla ya kufanya jambo.
Hizi ni baadhi tu ya piki piki zilizoegeshwa hapa ili kusubiri muafaka wa ulipishwaji ada ya kiasi cha shilingi 500 kwaajili ya parking uliokuwa ukitozwa na manispaa ya mji wa Arusha.
Afisa wa polisi akitoa muongozo kwa waendesha piki piki waliogomea ulipishwaji wa ada ya parki ambayo hawaelewi kuidhinishwa kwake.
Baadhi ya waendesha piki piki wakiwa na askari wakati wa mgomo huo.
Takribani piki piki 1000 zilikuwa zimepaki katika eneo hili la Silent Sakina mjini Arusha wakipinga ulipishwaji wa ada ya shilingi 500 ya parking.
Umati wa waendesha piki piki ulifurika katika eneo la Silent Sakina mkoani Arusha.
Ndani ya banda hili maeneo ya Silenteen ndipo kikao hichi kilikuwa kikiendelea kati ya waendesha piki piki na viongozi wa kiserikali.
Mgomo huo ukiwa ndani ya mazungumzo mazito na viongozi wa serikali, huku wengine walichangamkia biashara ya viatu iliyokuwa hapo jirani.