All rights reserved to Asili Yetu.
 |
Huyu ndiye Dj Calvy aliyeipagawisha crew ya XXL ya Clouds Fm mjini Arusha. |
Huyu ndiye Dj Calvy aliyewapagawisha crew ya XXL ya Clouds Fm mjini Arusha katika studio za Clouds tawi la Arusha.Mastaa wa XXL yani B12, Adam Mchomvu na Nchakali wakiwa katika kipindi cha redio kilichokuwa kinahusiana na mashindano ya kuwasaka wasanii wa Fiester watakaoenda Dar es salaam kuchuana na washindi kutoka mikoani, kilibamba sana baada ya Adam kumpatia nafasi Dj mdogo mwenye umri wa miaka 16 kusimama katika mashine na kuwaacha midomo wazi mastaa wa XXL.
Baada ya kuwa Calvy amepewa kugonga ngoma 4 jamaa waligundua kipaji chake na kutoa tamko la kumpatia ofa ya kumlipia usafiri wa kwenda na kurudi na huduma zote siku ya BRITHDAY yake ili akasababishe katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm jijini Dar es salaam.
 |
DJ Calvy akiwa katika pause pande za A Town. |
 |
DJ ALI (CLOUDS FM ARUSHA)- Huyu ndiye aliye tengeneza kipaji cha Dj Calvy hadi leo kimeonekana katika crew ya XXL ya Clouds Fm ya Dar. DJ ALI ambae pia ndie kiongozi wa FURAHIA DJ kutoka Arusha amekuwa ni msaada mkubwa kwa maDJ wengi wanaochipukia mjini Arusha. |
 |
MACHOTA (kushoto) akiwa na DJ CALVY baada ya mida ya kazi A Town. |