AKAMATWA NA SEHEMU ZA SIRI ZA MPWA WAKE.
Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini amekamatwa baada ya
kupatikana akiwa na sehemu za siri kwenye pochi lake ambazo zinaaminika kuwa za
mpwa wake ambaye hajulikani aliko.
Msemaji wa polisi, aliambia BBC kuwa babada ya kukamatwa
kwake , mwanaume huyo aliwapeleka maafisa wa polisi kwenye msitu katika mkoa wa
Eastern Cape, ambako mwili uliokatwakatwa ulipatikana.
Kichwa cha msichana huyo pamoja na miguu yake ilikuwa
imekatwa na zilipatikana karibu na kiwiliwili chake.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 42, anatarajiwa kufikishwa
mahakamani kwa kosa la mauaji.
Mmwanaume huyo alishtakiwa baada ya kushukiwa kuhusika na
kutoweka kwa msichana huyo mwenye umri wa miaka 18, aliyepotoea katika mji wa
Ngcobo siku ya Jumapili.
Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela alisema kuwa sehemu hizo
za siri, zilipatikana ndani ya pochi lake.
Alisema sababu ya kuuawa kwa msichana huyo haijulikani na
kwamba uchunguzi unafanyika.
Alipoulizwa ikiwa mauaji hayo yanahusishwa na waganga ambapo
sehemu za mwili wa watu hutumiwa kwenye madawa yao, bwana Fatyela alisema kuwa
hawezi kubaini hilo kwa sasa.
Kumekuwa na visa vingi vya kuuza sehemu za siri za watu
katika sehemu nyingi za Afrika kwa sababu sawa na hizo.
Afrika Mashariki imeshuhudia visa vingi vya kuuawa kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi au maalbino, huku sehemu za miili yao zikikatwa kwa
sababu za kishirikina.
Mwanaume huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA