All rights reserved to Asili Yetu.
'EMINEM'
Ingawa ni mara chache kwa msanii Eminem kuvuma kama wasanii wengine walivyo katika soko, lakini miezi michache iliyopita imethibitika kuwa ndiye msanii maarufu anayeongoza kwa kupendwa "Liked" katika mtandao wa Facebook. Page ya Facebook ya Rapper wa I'm not afraid" kwa wiki moja tuu, watu 179,000 hubonyeza kitufe cha 'LIKE' (kupenda).
Kutokana na matokeo hayo msanii Eminem ameongoza wasanii wenzake kwa kupendwa na watu milion 60 katika mtandao wa kijamii.
Takwimu zimezidi kuonyesha kuwa katika ukurasa wa msanii Eminem kuna "Like" milioni 60.1 na huku akifuatia msanii Rihanna akiwa na watu waliobonyeza kitufe cha "Like" milioni 59.4, akifuatia Lady Gaga na mashabiki milioni 53 na msanii wa "I Believe" au "Boyfriend" Justine Bieber wakibonyeza kitufe cha "Like" watu milion 45.7
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa msanii Eminem katika page yake ya Facebook kuwa na mashabiki wanao "Like" 179,000 kwa wiki, lakini katika mtandao wa Twitter mambo yako kinyume.