Tuesday, April 22 2025

Header Ads

Breaking News
recent

TOP 10 YA MATATIZO YANAYO WAKABILI VIJANA KWA SASA.

All rights reserved by Victor Machota.


10:  MAGONJWA:
Kwa kiwango kikubwa magonjwa yamekuwa ni mengi sana kwa binadamu wa wasasa....hususani tukiangalia kwa upande wa vijana wanakabiliwa na magonjwa mbali mbali kama ugonjwa wa Ukimwi, magonjwa ya zinaa,malaria, ugonjwa wa macho, meno n.k. Vijana wengi wanapoteza maisha hata kuliko wazee, swala hili haliko tuu hapa kwetu Tanzania, bali ni dunia nzima.Ili wewe kijana uweze kutimiza malengo yako, inakubidi uishi maisha uliyopewa kwa kujilinda. Hakuna anayekulinda bali wewe mwenyewe na Mungu wako.

9:  POMBE
Hii imekuwa ni sehemu ya maisha kwa vijana wengi wa sasa. Maisha yanayo hatarisha maisha ya familia zao au watu wanao wategemea kwa namna moja au nyingine.Unywaji wa pombe husababisha madhara makubwa sana katika mwili. Na kwa sababu hii, pombe yote mtu anayokunywa hupita katika seli za Ini na zinajaribu kuiondoa, lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zina kufa.
Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado zitaendelea na maisha, ila mwisho wake Ini linashindwa kufanya kazi na kujikuta njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba.

8:  MAVAZI
Kwa asilimia kubwa ya vijana wa leo ni wasafi na wanajari miili yao, isipokuwa wengi wao hujikuta wakipata shida kisaikologia kufuatia mitoko hasa ya vijana wa kike wanapoamua kuvaa nusu au robo mwili (mitindo ya kimagharibi) kitu ambacho huhamasisha kufanya vitendo vya ngono.Vijana wengi wamezama katika dimbwi hili, kwa mfano wiki hii kule Afrika ya kusini wanawake waliandamana kupinga uvaaji wa nguo ndefu, inamaana wanahitaji nguo fupi.Kijana, tunza mwili wako, mwili hauna spea.

7:  MOVIE / FILAMU
Sela na katiba au sheria za nchi za magharibi zinatofautiana sana na za Afrika, hivyo vijana wengi wanajikuta wakitaka au wakitamani kuishi maisha ya kimovie au wakitaka kuwa kama mcheza movie flani.Yule ameigiza tu, huenda yale siyo  maisha yake, ni ya kwenye filamu tu. Movie nyingi  za sasa kutoka nje, ukiangalia hazikosi ngono ndani yake hadi za jinsia moja.Hivyo vijana tuishi maisha yetu wenyewe, tuwe ma roll model wa maisha yetu na siyo ya movie.

6:  ELIMU
Vijana wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi na ngumu kielimu hasa pale inapofika wakati wa kulipa ada.Ukitaka kujua ugumu wa elimu nenda kawaulize vijana walioko vyuoni, hasa vyuo vikuu. Asilimia kubwa ya vijana kila kukicha wanalilia mikopo kutoka serikalini.Serikali nayo nivyema sasa ikaangalia vijana wasiyo jiweza kwa kipato, basi ikawawezesha mikopo kuliko kufanya maandamano na kupoteza muda wa masomo.

5:  AJIRA
Vijana wengi wako ndani ya hili dimbwi la kutafuta ajira, na wengi wao huikosa kutokana na mfumo na hali ya uchumi iliyopo, pamoja na teknlogia mpya.Hivyo kazi nyingi zinahitaji elimu na ujuzi pia.Asilimia kubwa ya vijana ni ambao hawana ajira, hii inasababishwa na umasikini wakutokuwa na mitaji ya kuweza kujiajiri wenyewe.Hata pia vijana wanao maliza elimu ya juu, wanakabiliwa na ukosefu huu wa ajira, kwa mfano; kijana akienda kuomba ajira sehemu, wanamwambia wanahitaji mtu mwenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu.Je, waliomaliza masomo kwa wakati huo watapata wapi uzoefu wa kazi, kama sio kuupata wakiwa kazini?

4:  MAADILI YA DINI
Hili ni jambo moja muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, kumuabudu, kumuheshimu na kufanya mapenzi yake Mwenyezi Mungu.Idadi kubwa iliyoko makanisani na sehemu nyingine za ibada ni vijana.Lakini vijana wengi hususani wa kike, wamejikita katika mavazi yasiyoendana na sehemu za ibada,"utakuta kijana wa kike amevaa kisketi kifupi na kuacha sehemu husika wazi, kiasi kwamba kwa bahati mbaya akidondosha kitu chini itakuwa vigumu kukiokota.Vijana tuwe macho katika hili, kwasababu pale ni sehemu takatifu na ya mwisho hapa duniani kumuonyesha Mwenyezi Mungu unyenyekevu wote ili tusamehewe na tujaaliwe maisha mazuri.

MPENDWA MSOMAJI UNAWEZA KUANDIKA MAMBO (MATATU) YALIYOBAKIA KATIKA ORODHA HII, ALAFU MIMI NITAYAWEKA. ANDIKA KATIKA KIBOKSI HICHO HAPO CHINI CHA COMMENTS.

Leave a Comment

Powered by Blogger.