Tuesday, May 13 2025

Header Ads

WHITNEY HOUSTON MAZISHI YAKE YATAONYESHWA LIVE!

All rights reserved by Victor Machota.

Kanisa alilokuwa akiimba msanii Whitney Houston wakati hajaingia katika muziki wa kidunia.Hapa ndiyo sala yake ya mwisho itakapofanyika siku ya Jumamosi.
Mamilioni ya wapenzi na mashabiki wa msanii Whitney Houston aliyefariki katika hoteli ya Beverly Hills nchini Marekani siku ya Jmosi Februari11, 2012, hawataweza kuhudhuria mazishi ya msanii huyo  yatakayofanyika  New Jersey on Sunday, February 19, 2012 na hivyo wataweza kuangalia mazishi hayo live kupitia "homecoming" service yake kupitia mtandao wa Internet. 

Habari kutoka kwa msemaji wa Whitney, 'Kristen Foster' zimesema kwamba, The Associated Press itaruhusiwa kuchukua video za mazishi siku ya Jumamosi huko Newark.Chombo cha Associated watakuwa wakionyesha live mazishi hayo kupitia link ya http://livestream.com/aplive.Tukio hilo pia litakuwa katika vyombo mbali mbali kupitia satellite.

Mwilili wa Whitney Houston wakati ukiwasili uwanja wa ndege wa  Teterboro siku ya J3, 13, 2012 watu walifurika wakiwa na mauwa, japokuwa mazishi hayo yatakuwa ni kwa mwaliko maalum tu.Taarifa zinasekma kuwa Whitney Houston atazikwa pembeni mwa kaburi la baba yake mzazi John Russell Jr, aliyezikwa pale miaka tisa iliyopita.

Kaburi la baba yake Whitney Houston.

Leave a Comment

Powered by Blogger.