Wednesday, April 23 2025

Header Ads

WAIGIZAJI WALIOKUMBANA NA JOTO LA TAMTHILIA YA WALANG HANGGAN - MY ETERNAL.

Tamthilia ya My Eternal ni moja ya Tamthilia zilizobamba sana mashabiki wa movie hapa nchini na kuweza kufuatiliwa na mamilioni mara kwa mara. Hawa ni baadhi ya wahusika wa Tamthilia waliokumbana na msoto wa maisha katika Tamthilia hiyo.

Nikianza kushoto ni mama yake Nathan au mke wa Marco Montenegro, yeye alikumbana na changamoto kibao mojawapo ikiwa ile ya kuolewa na Marco Montenegro na kusababisha penzi la Emily na Marco kuishia pabaya. Changamoto nyingine ni pale alipogundua kuwa Daniel ni mtoto halisi wa mumewe Maroco na pia Emily aliporejea mama huyu hakuwa na amani kabisha na hadi mwisho wake aliuwawa na Miguel.

Nathan (wa pili kutoka kushoto) yeye alivaa changamoto za maisha pale alipompenda msichana mrembo Katarina, na kuingia katika uwanja wa marumbano na Daniel. Nathan alikuwa akichukia sana anapomkuta Katarina akizungumza na Daniel, japokuwa kiukweli Nathan alilazimisha penzi kwa Katarina. Lakini kikubwa zaidi ni ambapo alifunga ndoa na Katarina na baadaye akaja kuambiwa ndoa ile ilikuwa batili. Tuliona hadi mwisho Nathan aligeuka kuwa kichaa kutokana na mzongo wa mawazo.

Johanna (wapili kutoka kulia) yeye alipenda asikopendeka, muda mwingi alikula kwa macho kwani aliye mpenda alikuwa tayari alikwisha penda kwingine. Johanna alikuwa ni binti mzuri na mrembo pia, lakini hakujua mapenzi hayalazimishwi, alimpenda sana Daniel, lakini Daniel alikuwa tayari akimpenda Katarina.
Ameigiza kama Johanna.
Thomas (wa mwisho kulia) yeye alionja joto ya jiwe mara kadhaa alipokutana na Daniel. Thomas alipewa na pesa na baba yake akidai kuwa anahitaji kujitegemea na kufungua kampuni yake, baba yake alimpatia pesa, lakini Thomas alienda kucheza kamali na kuliwa pesa zote na kudaiwa nyingine zaidi kitu kilichosababisha baba yeke kufariki kwa ugonjwa wa moyo. Lakini pia siku mbaya kwa Thomas ni pale alipofungwa mikono na Daniel alafu Daniel akawasha gari na kumfuata kwa kasi akimtishia kumgonga, duh.. jamaa ilibidi ajikojolee kama mtoto vile.

Tukutane tena katika dondoo nyingine za mataa wa Tamthilia ya Walang Hanggan - My Eternal.. Karibu Asili Yetu Tanzania blog.

Leave a Comment

Powered by Blogger.