Saturday, July 26 2025

Header Ads

KISANDUKU CHEUSI KINACHOTUNZA TAARIFA ZA MELI CHAPATIKANA.

All rights reserved by Victor Machota.


Hii ndio meli ya kiitaliano iliyozama katika bahari ya Mediterranean katika  ufukwe wa "Concordia" uitaliano, umbali wa mita 300 kufika ufukweni, ikiwa ni baada ya kugonga mwamba na kuzama.
Watu sita walifariki baada ya kushindwa kuogelea, lakini chakushangaza wapo walio kabiliana na joto lenye nyuzi joto 57 la bahari wakati wa usiku na kuweza kujiokoa.

Watafiti wa majini wa nchi hiyo wamekipata kisanduku kidogo cheusi kinachotunza taarifa zote za meli hiyo kubwa iitwayo Concordia. Meli hiyo ilikuwa imebeba takribani abiria 3,200 pamoja na wafanyakazi wa meli hiyo takribani 1000 na tani 2,300 za mafuta juu ya bodi ya meli hiyo.

 Captain wa meli hiyo bwana "Schettino" anashikiliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo, ambapo kwa sasa maafisa upererezi wamekwisha wahoji mashahidi zaidi ya100 wakiwemo abilia wa meli hiyo pamoja na wafanyakazi wa meli hiyo.Bwana Schettino atahukumiwa kifungo cha miaka 15 iwapo atapatikana na hatia.Mpaka sasa report rasm za kisanduku hicho hazijatolewa, hivyo fuatilia hapa hapa Asili Yetu blog kwa taarifa zaidi.



Leave a Comment

Powered by Blogger.