KISHINDO TZ: Fahamu nchi yenye piramidi nyingi kuliko nchi zote duniani
Mguu wa KISHINDO TZ unanyanyuka na kutua nchini Sudani, kumekuwa na historia kibibilia za piramidi za Farao kule Misri, kweli ni maarufu sana, lakini bado kuna kinara wa mapiramidi (minara) kote dunia.
Sasa habari zikufikie wa kwetu, sio tu kwamba Sudan ina piramidi nyingi kuliko Misri, lakini fahamu kuwa idadi ya piramidi za Misri hata hazijakaribia za Sudani. Wakati piramidi takribani 138 zikigunduliwa nchini Misri, Sudan inajivunia kuwa na takribani piramidi 255.
Fuatilia KISHINDO TZ kwa mengine ya ajabu zaidi.