All rights reserved by Victor Machota.
Baada ya kufanya utafiti wa kina juu ya uhusiano uliopo
kati ya mwenye nyumba na mpangaji,
nikianzia Songea 2005 na kumalizia Mwanza 2011,
sasa nakuletea riwaya ya kisayansi(science fiction).
"HASIRA ZA MPANGAJI" ni riwaya iliyotungwa na mimi Gabriel Nombo.
Inaelezea maisha ya watu kwenye sayari iliyo
nje ya mfumo wa jua, extrasolar planet. Sayari yenye watu
wanaopanga na wanaopangisha nyumba kama watu wa hapa duniani.
Tofauti ni kwamba, wao wameendelea zaidi kisayansi na kiteknolojia
ukilinganisha na sisi wa duniani.Pia, kwa asili binadamu
wa huko (aliens) wana hasira sana. Kwenye nyumba wanazoishi mifarakano
ipo muda wote. Kitu kidogo tu, kwa wao, chaweza zua hasira
kubwa. Tafadhali usiikose riwaya
hii ya aina yake. Ipo njiani kukutembelea.
Kwa maoni au maswali, tafadhali nitumie barua pepe."Gabriel Nombo" <mapigaby@yahoo.com>