All rights reserved by Victor Machota.
Wakati wa uhai wake jana akiwa anahudumiwa na muuguzi. |
Mwigizaji
wa siku nyingi Tanzania, Mzee kipara amefariki leo kwenye nyumba ya
KAOLE SANAA GROUP ambapo alikua anaishi, kutokana na maradhi mbalimbali
pamoja na utu uzima ambapo alianza kuugua zaidi ya mwaka mmoja
uliopita.
Mzee
Kipara alikua miongoni mwa waanzilishi sita wa KAOLE SANAA GROUP mwaka
1999, ambapo wengine ni Marehemu RAJABU HATIA (MZEE PWAGU), MAMA
HAMBILIKI, Bi HINDU, ZENA DILI, CHRISANT MHENGA ambapo mchezo wa kwanza
wa kikundi hicho kuoneshwa ITV, uliitwa HUJAFA HUJAUMBIKA ambapo Mzee
kipara alikua anacheza kama Baba mzazi wa DR CHENI wakati huo Dr CHENI
anataka kumuoa KISSA ambae alikua binti mlemavu.
kabla
ya kifo chake, mwigizaji huyo alishazushiwa kifo zaidi ya mara moja,
ambapo mara ya mwisho ilikua ni NOVEMBER 10 mwaka jana.
Mwili wa Mzee KIPARA utazikwa kesho Kigogo Dar es salaam , kwa mujibu wa mwenyekiti mstaafu wa KAOLE Sanaa Group CHIKI.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA