All rights reserved by Victor Machota.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta amesema
video inayoonyesha askari wa jeshi la majini la Marekani wakikojolea
maiti za Wafghanistan ni la "kusikitisha sana".
Alisema, wale walioshiriki katika tukio hilo kwa namna moja au nyingine watachukuliwa hatua "kali sana".Chanzo cha video hiyo hakijajulikana.
Bw Panetta amemwamuru kamanda wa Marekani na majeshi ya Nato nchini Afghanistan, Jenerali John Allen, kuchunguza suala hilo.
Katika taarifa yake, Bw Panetta alisema aliona video hiyo.
"Tabia hii kwa hakika inasikitisha sana. Tabia hii haikubaliki kabisa kwa wote walio kwenye jeshi la Marekani."
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Pentagon imesema inachunguza uhalisia wa video hiyo, lakini hakuna lolote kuashiria kuwa video hiyo si halisi.
Bw Panetta hakukana uhalisia wa video hiyo.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA