PICHA NA SAUTI YA "MH. NAMELOK SOKOINE" AKIWASHUKURU WATANZANIA NA VIONGOZI WOTE KWA KUSHIRIKI SIKU YA KUMBU KUMBU YA BABA YAKE HAYATI "EDWARD MORINGE SOKOINE" MONDULI ARUSHA.
Mh. Namelok Moringe Sokoine - Mbunge wa viti maalum CCM akikabidhiwa cheti cha kushiriki mbio za Edward Moringe Sokoine Mini Marathon na mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mlongo jana Wilayani Monduli Arusha.
Namelok Sokoine ni binti wa hayati Edward Moringe Sokoine ambaye ni mfano wa kuigwa na wanawake wote nchini kwa kusimama kidete katika maandalizi ya kumbu kumbu za baba yake, aliyefariki mnamo tarehe 12/4/1984 kwa ajali ya gari wakati huo akiwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dada huyu ni mchapa kazi, anapenda watu wote bila kujali cheo, kabila au kitu chochote alichonacho. Namelok Sokoine amewashukuru viongozi na watu wote waliohudhuria katika kumbu kumbu ya hayati waziri mkuu Edward Moringe sokoine na kutoa ahadi ya kuwakaribisha tena mwaka kesho kushiriki tukio hilo ambapo watakuwa wakiadhimisha miaka 30 tokea Edward Sokoine afariki dunia.
Mgeni rasmi atakuwa Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ambapo pia kutakuwa na mbio za kilomita 42.
Mengi zaidi msikilize hapa chini......

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA