WAPENZI WA TAMTHILIA YA MARA CLARA WAINGIWA NA SMANZI KATIKA "EPISODE" YA 42.
Mchezo unaorushwa na kituo cha Staa Tv unaendelea kuchukua
sura mpya baada ya kufanyika mazishi ya Mara, mmoja wa washiriki waliokuwa
wakikonga nyoyo za mashabiki wengi.
![]() |
| MARA |
Familia zote mbili zinazama katika dimbwi zito la kumpoteza
binti yao, lakini siri nzito yazidi kutanda kati ya Gurly (baba wa sasa wa
Clara) na washirika wake. Lakini pia polisi kama wameshtukia hivi mchezo
unaoendelea, sasa wamtaka Clara kwa uchunguzi zaidi kuhusu kifo cha “Mara”,
baba yake Clara hayuko tayari kuwakabidhi makachero wa polisi binti yake.
Kwa upande mwingine Clara anaanza kuchukua uwazi wa Mara
kuwa karibu na mama yake wa zamani “Avira” na kumuahidi atakuwa nae karibu siku
zote. Amenthe anarejea nyumbani usiku anamkuta Clara amelala na mama yake wa
zamani “Avila”, hakubaliani na suala hilo anaamua kumrudisha kwao.
Japokuwa Clara na Gurly (Baba yake) waliweka agano na siri
nzito ya kuzidi kummaliza Amanthe (Baba yake Mara) na kumtaifisha Avira, sasa
mambo yaanza kuvuja wazi wazi baada ya makachero wa polisi kumfuata Clara
wakitaka aongozane nao ili akafanyiwe mahojiano. Gurly anawazuia lakini Clara anapaza sauti kuwa “hapana
nitaongozana nao na nitawaeleza yote bila kuwaficha” baba yake anabaki ameduwaa,
kwani Clara tayari amekwisha shtukia kuwa baba yake ndiye aliyehusika na mauaji
ya “Mara”.
Nini kitaendelea? Tazama Star TV na pia tembelea ukurasa huu
mara kwa mara kupata michapo ya tamthilia za mastaa hawa.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA