Header Ads

Breaking News
recent

SWIZZ BEATZ ANUNUA NAKALA 150 ZA ALBUM MPYA YA ALICIA KEYS INAYOITWA (Girl On Fire).

Alicia Keys na mumewe "Swizz Beatz"
Album mpya ya Alicia Keys iliyoingia sokoni siku ya Jumanne (Novemba 27) wiki hii, mume wa Alicia Keys; Swizz Beatz amekuwa mteja wa kwanza katika mauzo ya mwanzo wa mauzo ya album hiyo wiki hii.

Swizz Beatz katika kuwadhihilishia mashabiki wake kuwa yeye pia ni shabiki wa muziki anaofanya mke wake, ameamua kujichanganya sokoni na kununua kopi 150 za album ya "Girl On Fire" ya Alicia Keys.

The Super Producer Swizz alionekana akitweet ujumbe huu kwa mashabiki wake.. “Ok I might get stan of the year award! So what! I just got 150 copies to give out 2 fans.”
"Girl On Fire" ni album ya tano ya msanii Alicia Keys ambapo katika wiki hii anatarajia kuuza  nakala kati ya 150,000-175,000 katika wiki yake ya kwanza, japokuwa album yake ya nne "Element Of Freedom"aliuza nakala hadi 417,ooo.
Album hiyo iko sokoni na album mpya ya Rihanna inayoshika No. 1 spot ya Billboard baada ya album yake ya Unapologetic kuuza karibu nakala 240,000 mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.