RAIS WA KWANZA WA AFRIKA KUSINI NELSON MANDELA AFANYIWA UPASUAJI WA KIBOFU
![]() |
| Nelson Mandela |
Ikulu ya rais wa Afrika Kusini inasema kuwa Nelson Mandela
amefanyiwa uperesheni mjini Pretoria, kutolewa mawe ndani ya kibofu nyongo na
anasemekana anaendelea vizuri.
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka
94, alilazwa hospitali juma moja lilopita kutibiwa mapafu, na ukaguzi ukaonesha
mawe hayo kwenye kibofu.
Katika taarifa iliyotolewa na serikali, imearifiwa kuwa
madaktari waliamua kushughulika na mapafu yake Bwana Mandela kwanza, kabla ya
kufanyiwa upersheni wa Jumamosi.
Wakuu wa Afrika Kusini wamelaumiwa kuwa hawakuwa wakieleza
hali ya Bwana Mandela, ambayo imechochea wasi-wasi zaidi kuhusu afya yake.
Source: BBC Swahili

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA