WEMA SEPETU ALIVYONUSULIKA KUTEKWA NA WATU ASIOWAJUA.
MISS Tanzania 2006 ambaye pia ni mcheza filamu mkali Bongo,
Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alikumbwa na kizaazaa cha kutaka kutekwa na
watu wasiojulikana wakimtuhumu kuwatukana kupitia Facebook.
Akizungumza jijini Dar juzi, Wema alisema tukio hilo lilimtokea
Kijitonyama, Dar wakati akitoka kwenye mishemishe zake kuelekea nyumbani kwake.
Alisema alipofika maeneo hayo, gari asilolijua lilimpita na
kwenda kusimama mbele yake kisha wakashuka watu asiowajua na kuanza kumuuliza
ni kwa nini anawatukana katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
“Nilivyosikia wanasema Facebook, roho yangu ikatulia maana
najua kuna watu kama 37 wanaotumia jina langu na picha zangu kwenye Facebook,
nilishuka kweye gari na kuanza kuwaelewesha kuhusu hilo, bahati nzuri walinielewa,” alisema
Wema.
Source: Hazuu blog

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA