VIDEO QUEEN, AGNES JELARD "Masogange" AMEMUWEKA WAZI MPENZI WAKE.
VIDEO Queen, Agness Jelard ‘Masogange’ hivi karibuni ameamua
kumuanika mpenzi wake aitwaye Evance Komu kupitia mtandao wa BBM.Masogange
alifanya hivyo kwa kutundika picha zinazomuonesha akiwa kimahaba na mwanaume
huyo kisha kusindikiza na maneno yasemayo; ‘mke wa Komu’.
Aidha, msanii huyo amemlalamikia mtu mmoja aliyejipachika
jina la Agnes kisha kufungua akaunt kwenye facebook na kuweka picha zake na
kuwatongoza wanaume.
“Nimechoshwa na huyu mtu, nikimbaini kweli nitamuumiza kwani
ananishushia hadhi yangu, mimi nina wangu najiheshimu, siwezi kujiuza
mtandaoni,” alisema Agness.
Evance alianza kupata umaarufu miaka kadhaa iliyopita baada
ya kujitosa katika tasnia ya filamu Bongo ambapo alianza kucheza filamu ya Roho
Sita na Valentine Day zilizosumbua sokoni.
Source: Global Publishers.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA