Tabia za wanyama watembeao usiku zimebadilika
Siku hizi mamalia wengi wanatoka wakati wa mchana, lakini maisha ya
vizazi vyao vya nyuma yalikuwaje?
Kikundi cha utafiti cha kimataifa kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature Ecology & Evolution ikisema mamalia wa kale walitoka wakati wa usiku, na tabia hii ilibadilika baada ya dinosaur wasioruka kutoweka duniani.
Siku hizi mamalia wengi wanatoka wakati wa mchana, lakini wengi wao wanakosa baadhi ya uwezo muhimu ukiwemo uwezo wa kutambua rangi mbalimbali kama wanyama wengine wanaotoka wakati wa mchana.
Macho yao yanafanana zaidi na wanyama watambaazi na ndege wanaotoka wakati wa usiku.
Baadhi ya watafiti wamekisia kuwa mamalia wa kale walitoka wakati wa usiku ili kuepusha dinosaur waliotoka wakati wa mchana.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza na Chuo Kikuu cha Tel aviv cha Israel wamechambua data za aina 2415 za mamalia wanaoishi sasa, ili kujua maisha ya vizazi vyao vya nyuma.
Uchambuzi umeonesha kuwa baada ya dinosaur wasioruka kutoweka duniani, vizazi vya nyuma vya mamalia vilianza kutoka wakati wa mchana, lakini mabadiliko hayo yaliendelea kwa muda mrefu sana wa mamilioni ya miaka.
Watafiti wamesema vizazi vya nyuma vya baadhi ya nyani wakiwemo sokwe na marmoset ni mmoja kati ya mamalia waliobadilisha tabia mapema zaidi.
Chanzo:CRI
PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA