Mwaka 2017 huenda ukawa ni kati ya miaka mitatu iliyovunja rekodi ya kuwa na joto kali
Mkutano
wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ulifanyika tarehe
6 mjini Bonn, Ujerumani.
Shirika la hali ya hewa duniani limetoa ripoti ikisema mwaka huu huenda utakuwa miongoni mwa miaka mitatu iliyovunja rekodi ya kuwa na joto kali licha ya kukumbwa na maafa za kimaumbile ikiwemo vimbunga, mafuriko, mawimbi ya joto na ukame.
Ripoti hiyo inasema kutokana na athari ya tukio la El Nino, mwaka 2016 huenda bado utachukua nafasi ya kwanza kwenye rekodi za miaka yenye joto kali, huku mwaka huu na mwaka 2015 itachukua nafasi ya pili na ya tatu.
Takwimu zinaonesha kuwa wastani wa joto duniani kuanzia Januari hadi Septemba mwaka 2017 ni kubwa zaidi kuliko wastani wa joto kati ya mwaka 1981 hadi 2010 kwa nyuzi 0.5 sentigredi, hii inamaanisha kuwa joto limeongezeka kwa nyuzi 1.1 sentigredi ikilinganishwa na kipindi cha mwanzo cha maendeleo ya viwanda.
Katika majira ya joto ya mwaka huu, siku zenye joto kali lillilovunja rekodi zilikuwa katika baadhi ya sehemu kusini mwa Ulaya, Afrika Kaskazini, Afrika Mashariki, Afrika Kusini na eneo la Russia lililoko barani Asia.
Chanzo:CRI
PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA