Header Ads

Breaking News
recent

Pango kubwa lisilojulikana lagunduliwa ndani ya piramidi la Khufu nchini Misri

 Piramidi la Khufu lililojengwa katika mwaka 2509 K.K. hadi 2483 K.K ni piramidi kubwa zaidi nchini Misri, linawavutia wanaakiolojia wengi kutokana na mambo mengi yasiyojulikana.

 Kikundi cha watafiti cha kimataifa hivi karibuni kimesema kimegundua pango kubwa lisilojulikana ndani ya piramidi hili.

Kikundi hiki kinachoundwa na watafiti wa Ufaransa, Japan na Misri kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature la Uingereza ikisema wamechunguza piramidi hili kwa teknolojia ya kupiga picha kwa chembe za Muon za miali ulimwengu, na kugundua kuwa kuna pango kubwa lenye urefu wa mita 30 na urefu wa kwenda juu wa mita kadhaa, ambalo linafanana na ushoroba ulioko chini ya piramidi.

Chembe za Muon za miali ulimwengu zinaweza kupita mawe, na zinapopita mawe au hewa, njia zao zinatofautiana, hivyo watafiti wanaweza kuthibitisha muundo wa piramidi kupitia njia za chembe hizi.

Watafiti wamesema bado hawajui umbo halisi la pango hili na linafanya kazi gani, lakini ugunduzi huo utawasaidia kuelewa zaidi piramidi hili na ujenzi wake.

Source: CRI

PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.

Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.