Nyangumi (samaki) husubiri samaki waingie wenyewe midomoni wakati wa mawindo
Wanasayansi wamegundua kuwa nyangumi aina ya Bryde wanasubiri samaki kuingia wenyewe midomoni baadhi ya wakati wanapokula.
Watafiti kutoka Japan na Thailand wametoa ripoti kwenye gazeti la Current Biology la Marekani ikisema hii ni mara ya kwanza kugundua njia hii ya kula, ambayo inaonesha kuwa nyangumi wanatumia njia tofauti ya kula katika mazingira tofauti.
Kwa kawaida nyangumi hao wanafungua midomo yao, kuogelea kwa kasi, na kumeza maji, samaki na kamba kwa pamoja, halafu wanafumba midomo na kutoa maji hayo.
Lakini watafiti walipochunguza vitendo vya kula vya nyangumi katika ghuba ya Thailand, wameshangaa kuona kuwa baadhi ya wakati waliweka vichwa vyao juu ya maji, na kufungua midomo yao, na kusubiri samaki kuingia midomoni.
Watafiti wameona nyangumi 31 wakila samaki kwa njia hii kwa mara 58.
Pia wamegundua kuwa wakati nyangumi wanapofungua midomo, samaki walioko karibu wanaonekana kupoteza uwezo wa kujua upande, na kuingia midomoni mwa nyangumi wakifuata mtiririko wa maji, na kwa wastani hali hii inadumu kwa zaidi ya sekunde 10.
Watafiti wamechambua kuwa njia ya kipekee ya kula huenda inatokana na mabadiliko ya mazingira.
Baadhi ya maeneo ya ghuba ya Thailand yamechafuliwa na kukosa hewa ya Oxygen, na kusababisha samaki na kamba wengi kuelea juu ya maji.
Chanzo: CRI
PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA