China inajenga uwanja wa ndege mkubwa duniani
China kwa sasa inajenga mojawapo ya uwanja mkubwa wa ndege duniani.
Uwanja huo mpya wa Beijing Daxing Airport inajengwa kwa gharama ya
bilioni 12 dola za Marekani na itakuwa uwanja wa ndege wa tatu katika
mji mkuu wa China, Beijing.
Mara tu baada ya kukamilika kwake, mradi huu mkubwa utaingia kwenye daftari za kumbukumbu kama uwekezaji wa miundombinu moja mkubwa zaidi chini ya uongozi wa rais wa sasa wa China Xi Jinping.
Mamlaka ya China imeweka wazi kuwa uwanja huo mpya wa ndege inaundwa ili awali iweze kushughulikia abiria milioni 45 lakini hatimaye kugonga abiria milioni 100 na tani milioni 4 za mizigo kila mwaka. Mji mkuu wa China ni nyumbani mwa watu milioni 23 kwa sasa.
Shughuli za ujenzi wa uwanja huo mpya zilizinduliwa mwaka 2014 na inatarajiwa kwa zitamalizika mwezi Oktoba mwaka 2019 wakati uwanja huo itaanza rasmi shughuli za usafiri.
Wazo la ujenzi wake ilitokana na msongamano unaoshuhudiwa katika uwanja wa Beijing Capital International Airport, BCIA na ule wa Beijing Nanyuan Airport, ambazo zote ziko katika mji mkuu, Beijing.
Vifaa vingine katika uwanja huo wa kisasa ni pamoja na hoteli ya kimataifa yenye vyumba 500.
Wafanyakazi katika mradi huo wanatumaini kumaliza kufunga pazia la kioo na paa la uwanja huo kabla ya mwisho wa 2017.
Eneo ambapo uwanja huo wa ndege umekalia ni mita milioni 7.5 mraba, sawa na viwanja 44 vya soka.
Wakati huo huo, mashirika ya ndege tayari yameanza kuhamia uwanja huo mpya na kuanza ujenzi wa ofisi zao. Barabara zinazounganisha hadi uwanja huo wa ndege tayari zimekamilika.
Ujenzi wa jengo hilo la kifahari linaendeshwa na makampuni ya ujenzi tatu na jumla ya wafanyakazi wa ujenzi 20,000.
Uwanja huo mpya wa ndege ni mojawapo ya maendeleo mahususi ya utawala wa Rais Xi Jinping, miaka 5 baada ya kuchukua hatamu uongozi wa nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.
Chanzo: cri
PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA