Header Ads

Breaking News
recent

China yasemekana ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na usafiri wa Treni za Chini

 CHINA ni nchi inayoongoza kwa kuwa na usafiri wa Treni za Chini (Subway)zinazotoa usafiri wa wananchi wake kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa utaratibu maalum jambo linalosaidia kupunguza msongamano barabarani katika nchi hii yenye idadi kuwa ya watu zaidi ya bilioni moja.

Mbali ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa usafiri huo wa chini ya ardhi,bado wanaendelea kupanua mtandao wa reli hizo kwa kasi hasa katika miji yake mikubwa ya Shanghai, guangzhoe, Beijing na Tianjin huku mwishoni mwa mwaka huu wakijiandaa kuanza kutoa huduma kwa kutumia treni za aina hiyo zinazojiendesha zenyewe (Automatic Tren).

Beijing ukiwa ni mji unaoongoza kwa kuwa na mtandao mpana wa reli nchini humo zilizoanza kutoa huduma 2002 wakati huo kukiwa na njia mbili tu lakini sasa wana njia 19 huku wakitarajia kuwa na njia 30 zitakazosafirisha abiria zaidi ya milioni 18.5 katika kilometa 999 ifikapo mwaka 2020.
Miji mingine kama Guangzhou ulioko katika jimbo la Guangdong ni ya nne kwa ujenzi wa mtandao wa Reli kwa njia ya kwanza ya reli hiyo ilianza kujengwa mwaka 1993 na kuzinduliwa rasmi miaka minne iliyofuata yaani mwaka 1997 ikiwa na njia tano.

Lakini mpaka kufikia mwaka jana ina njia kumi zenye uwezo wa kusafirisha watu milioni saba kwa siku na kwa kufanya kazi katika vituo 184 zenye km 260.5.

Katika kuongeza mtandao huo ,njia nne mpya zinajengwa huku nyingine zikipanuliwa hivyo kufanya baada ya njia zote kukamilika kufikia mwaka 2020 kutakuwa na kilometa zaidi ya 600.
Source: Radio China Kimataifa

PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.

Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
   

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.