Header Ads

Breaking News
recent

Nimeacha Youth Club watembelea watoto yatima na kuwapatia vifaa vya shule

Octoba 28 2017 stori ziliandikwa na umoja wa vijana wa NIMEACHA YOUTH CLUB baada ya kuona umuhimu wa elimu na ndoto za watoto walio katika mazingira magumu na yatima, na kuamua kujichanga na kukitembelea kituo cha MAKIMBILIO CHILD CARE kilichopo Kioga Arusha.
Vijana hao walitoa msaada wa vifaa vya shule, vifaa vya kulia chakula na baadhi ya vifaa vichache vitakavyowasaidia katika maisha ya kawaida.

Hata hivyo uongozi wa Nimeacha Youth Club umesema haya>>> "Tunapenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kukamilisha safari yetu ya kukitembelea kituo cha watoto yatima 'Makimbilio Child Care' kilichopo Kioga Arusha mnamo Tarehe 28/10/2017. 

Pia tunawashukuru sana wana NIMEACHA YOUTH CLUB kwa kujitokeaza pamoja na michango yao katika kufanikisha zoezi hili, Mungu awabariki na muwe na moyo huo huo katika jamii inayowazunguka. Asanteni"

PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
  

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.