Sayari mpya yagunduliwa, inauwezo wa kuwa na viumbe hai
Wataalamu wa anga za juu wamegundua sayari isiyo na joto sana na yenye ukubwa unaokaribia sana na wa dunia.
Mandhari katika sayari hiyo ambayo imepewa jina Ross 128 b yanaifanya kuwa pahala pazuri pa kutafuta viumbe au uhai anga za juu.
Sayari hiyo inapatikana umbali wa miaka 11 kwa kasi ya miali ya jua, na ndiyo sayari ya pili kwa karibu zaidi ambayo ina mazingira yanayokaribiana na ya dunia.
Sayari ya aina hiyo iliyo karibu zaidi hufahamika kama Proxima b, na wataalamu wanasema mazingira huko hayaonekani kuwa mazuri sana kiasi cha kuweza kuwa na viumbe.
Proxima b iligunduliwa 2016, na huzunguka kwenye mzingo ulio kwenye nyota kwa jina Proxima Centauri, ambayo hufahamika kama "nyota nyekundu mbilikimo".
Nyota hiyo huwaka sana na ina maana kwamba milipuko kwenye nyota hiyo huenda ikarusha miali nururishi yenye sumu kwenye sayari ya Proxima b.
Sayari hiyo mpya, Ross 128 b, huzunguka sayari ambayo haitofautiani sana na Proxima Centauri (pia ni nyota nyekundu mbilikimo), lakini hailipuki sana.
Chanzo: BBC
PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi. Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA