Tundu Lissu na tukio la upigwaji risasi Dodoma lawahuzunisha wengi
Ilikuwa Septemba 7 2017 ndipo habari zilipoanza kuenea katika mitandao mbalimbali ya habari na ile ya kijamii kuwa, Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu amepigwa Risasi Dodoma.
Watu wengi wameelezea hisia zao kuhusu tukio hili ambapo pia Mh. Lissu bado anapewa matibabu hospitalini, na mmoja kati ya watu walioguswa na tukio hili na kusema jambo ni Mh. Rais Magufuli ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika>>>
“Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka, Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria”>>> Rais Magufuli
Tunamuombea pia Tundu Lissu Mungu amponye. Amina