Header Ads

Breaking News
recent

Njia za kuishida hasira katika maisha

Kuwa na hasira ni hali ambayo inaweza kutokea wakati wowote katika maisha ya mwanadamu, ni hali ambayo huja pale tu mtu anapokuwa amesababishiwa na jambo flani au hali asiyoipenda.

Kila binadamu huwa na kiwango anachoweza kumudu hisia zake, kunawengine ni dhaifu katika kumudu hisia zao, ziwe hasi au chanya, na kunawengine wana vifua vya kumudu hisia zao, japo kila kitu kinawezekana endapo utaamua.

Ninaposema hisia hasi namaanisha zile hisia mbaya zinazokuijia na kukufanya uwe ni mwenye hasira, kwa mfano mtu amekutukana, amekudharau au amekudharirisha mbele za watu.

Hisia chanya ni hisia nzuri lakini zinazohitaji kiasi na wakati sahihi wa kuziruhusu kutumika, kwamfano umetumiwa sms kuwa umeshinda kiasi flani cha pesa, lakini uko kwenye kikao na wakuu wako wa kazi, je utapiga yowe, lah hasha! utapaswa kutunza hisia zako hadi utakapofika eneo sahihi la kutoa hisia zako.

Ukiangalia hata katika maandiko matakatifu, suala la hasira limezungumziwa pia, kwa mfano "Mtu wa hasira huchochea ugomvi". "Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano">>> Mith.15:18  

" Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hira mbaya huzirwa">>> Mith 14: 17 

"Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Mith 19:11

Hivyo kumbe hasira ni maamuzi ambayo yako chini ya mtu na anauwezo wa kuimudu hasira atumiapo busara.

Siri ni kwamba unapaswa uwe na busara pale unapoona umekwazika, chukulia rahisi tu pale unapokuwa umekwazwa na jambo flani, onesha kutokulijali na hapo utakuwa umeiepuka hasira.

Lakini pia njia nyingine rahisi unazoweza kuzitumia unapokuwa katika hasira ni hizi; chukua muda angalia movie kama wewe ni mpenzi wa movie, lakini zisiwe zenye huzuni maana zitakuongezea hasira zaidi, soma vitabu vya dini au novel stori, sikiliza muziki, tembelea marafiki au hata fanya mazoezi ya kukimbia au yoyote yale. 

Hayo na mengine mengi yatakufanya usiingie hasara maana wahenga walisema 'hasira hasara', zipo hasara nyingi zinazosababishwa na hasira, mojawapo ni ile ya kiafya, kifedha na hata kupoteza maisha au kuwa mlemavu katika mwili wako.

Chunga sana hasira isije kutawala, iogope  hasira maana Mwenyezi Mungu pia hapendi.

Tukutane tena wakati mwingine katika makala fupi za Maamuzi katika Maisha, fanya maamuzi sahihi ishinde hasira.

SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.