Zimetajwa nchi 10 zinazoongoza kwa usafi wa mazingira duniani ingawa zina idadi kubwa ya watu.
Kuwa na mazingira masafi ni jambo jema katika afya ya mwanadamu, japo sii jambo rahisi tu sehemu ya watu wengi kuonekana safi, hii bado ni changamoto kwa nchi nyingi duniani.
Sasa nakusogezea orodha ya nchi 10 zinazotajwa kuwa na mazingira masafi licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, orodha hii ni kwa mujibu wa Environmental Performance Index .
10: Norway
Norway ni nchi ya kumi kwa kuwa na mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na mazingira machafu kwa zaidi ya asilimia 78.04
9: Sweden
Sweden inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na uchafu kwa zaidi ya asilimia 78.9

8: Austria
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi
zenye amani duniani Austria inatajwa pia kuwa moja ya nchi yenye
mazingira safi na imeshika nafasi ya 8 kwa mwaka 2017.
7: Spain
Kwa mujibu wa Environmental
Performance Index Spain imeshika namba saba kati ya nchi zenye mazingira
masafi ambapo imeweza kupambana na uchafu kwa zaidi ya asilimia 79.79
6: Germany
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi
inazotembelewa kwa wingi lakini hii haifanyi ujerumani kuwa nchi
chafu,kwani mwaka 2017 imeweza kushika nafasi ya sita miongoni mwa nchi
safi zaidi duniani.
5: Czech Republic
Czech Republic imeshika namba
tano kati ya nchi zenye mazingira safi kwa mwaka 2017 kwa mujibu wa
ripoti ya Environmental Performance index .
4: Singapore
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi
zinazotajwa kama kitovu cha biashara duniani Singapore pia ni moja kati
ya nchi yenye mazingira masafi ambapo imeweza kupamba na uchafu kwa
zaidi ya asilimia 81.78.
3: Australia
Australia imeshika namba tatu kwa
nchi zenye mazingira masafi kwa mwaka 2017 na kwa mujibu wa
Environmental Performance index Australia imeweza kupambana na mazingira
machafu kwa asilimia 82.4.
2: Luxembourg
Environmental Performance imeipa
Luxembourg asilimia 83.29 na kuifanya kuwa nchi ya pili kwa mwaka 2017
kuwa na mazingira masafi duniani.
1: Switzerland
Switzerland ni miongoni mwa
nchi zenye mazingira masafi duniani ambapo wameweza kupambana na
mazingira machafu kwa zaidi ya asilimia 87.67 ,kwa mujibu wa
Environmental Performance Index Switzerland ni miongoni mwa nchi zenye hewa safi.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA