Inasemekana kuna viambata milioni 10 vya hewa ya sumu katika magari mapya.
Watu wengi wamekuwa wapenzi wa magari mapya jambo ambalo huwafanya
kufuatilia kwa karibu kila wanaposikia kuna aina mpya ya gari imeingia
sokoni, lakini magari mapya yanadaiawa kuwa na athari mbaya kwa afya.
Kwa mujibu wa utafiti ni kwamba wamiliki wa magari wako hatarini sana baada ya kubainika kuwa huvuta hewa yenye viambata 10 million vya
sumu katika kila pigo moja la kupumua wakiwa garini huku ndani ya
magari mapya pekee kukiwa na viambata vya sumu mara 10 zaidi ya magari
ya zamani.
Mmoja wa waliofanya jaribio hilo Nick Molden kutoka Emissions Analytics alisema:
“Madereva na abiria wao wanaweza kuathirika sana kama wapo garini.
Viambata hivyo ni vidogo sana – ambavyo sio rahisi kuonekana, lakini
kukaa kwake muda mrefu ni mbaya kwa afya ya madereva.”
Jaribio lilifanywa kwa kuhesabu viambata vilivyochafuliwa kwa cubic centimetre
ya hewa kwenye magari kwa zaidi ya saa nne katika uendeshaji wa mjini
na kijijini ambapo ilibainika kuwa, hewa ya kawaida ina vijidudu, chavua
na vumbi, lakini kiwango kidogo ni hatari kwa afya ukilinganisha na
masizi yatokayo kwenye engine – hasa diesel.
Prashant Kumar, Professor wa Uhandisi wa Kimazingira katika Chuo Kikuu cha Surrey alisema: “Kama utasimama kwenye taa za barabarani ukiwa umejifungia vioo, sumu hii inakuwa kwa kiwango kikubwa.”
Source: Millardayo

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA