Header Ads

Breaking News
recent

"UTAMU" TAMTHILIA YA WALANG HANGGAN (MY ETERNAL) SASA NI MAJANGA - DANIEL NA MAMA YAKE EMILY MATATANI.

Kwa wapenzi wa Tamthilia ya My Eternal sasa yafika patamu baada ya kifo cha mke wa Marko Montenegro sasa tuhuma nzito zatawala kila kona ya familia ya Emily Gidoti akituhumiwa kuhusika katika kuiripua ndege aliyokuwa amepanda mke wa Marko Montenegro.

Baada ya Emily kukamatwa na polisi na baadae kutolewa kwa dhamana, sasa mikosi yamgeukia mwanae Daniela Gidoti ambaye anaonekana kuchimbua undani wa mauwaji ya mama yake Nathan. Ukweli ni kwamba aliyepanga mauwaji ya mama yake Nathan japokuwa lengo likiwa ni kumuua Emily Gidoti ni mama yake Marko Montenegro yani Margret akisaidiwa na Miguel ambaye ni mtu wa karibu na Emily.

Tayari Daniela amemshitukia Miguel  na kuanza kumchunguza, lakini Miguel naye anashtukia mchongo huo, sasa apanga njama ya kumbambikizia kesi ya mauwaji na kumtupa jela kwa muda usio julikana.

Katika upande wa kueleza hisia za mwili ya mapenzi, Johan Montenegro anamweleza Daniela jinsi anavyomuhusudu lakini Daniela anakataa kwasababu anajua ni msala tu. Lakini Johan anamua kunywa pombe na kurudi nyumbani akimtomasa tomasha Daniela. Daniela anaamua kumuweka kitandani na kumfunika shuka kisha kutoka nje. Lakini wakati akitoka chumbani huku vishikizo vya shati vikiwa wazi, Nathani alishtushwa na hali ile na kuamua kumuita baba yake ambapo walijua jamaa amekwisha fanya mambo.

Ukweli ni kwamba Daniela hakufanya chochote na Johan, isipokuwa Johan alipoulizwa alimwaambia hakumbuki chochote kama walifanya, ila aliwaambia kuwa yeye amekwisha kuwa na anamtaka Daniela.

Daniela akiwa njiani kuelekea alikokuwa akienda, mara anapokea simu ya mlinzi wa mama yake akimtaka arejee nyumbani kwani tayari majambazi walikuwa wakimuwinda, akiwa bado anajibu simu jambazi aliyeirpua ile ndege kwa bomu, akamkaba shingo kwa nyuma lakini kama kawaida Daniela alimkabidhi kichapo cha mbwa mwizi hadi polisi walipofika na kumchukua jambazi huyo.

Marko Montenegro anaamua kwenda kumuhoji jambazi aliyekamatwa, lakini badala yake anakaa pembeni na kumsikiliza polisi akimuhoji jambazi. Jambazi baada ya kubanwa vilivyo anaamua kumsingizia Daniela Gidoti kuwa ndiye aliyeiripua ile ndege na kupanga kusambaratisha familia ya Montenegro. Polisi wanaagizwa kumkamata Daniela.

Lakini Damu ni nzito kuliko maji baba yake Daniela yani Marko Montenegro anaamua kumpigia Emily Gidoti na kumwambia kuwa polisi wanamfuta Daniela. Emily anamsihi Daniela atoroke na ili apate muda mzuri wa kupeleleza mauwaji ya mama yake Nathan.

Polisi wanamsaka Daniela kwa hali na mali, huku nyuma mama yake wamemkamata tena kwa kumficha Daniela. Miguel naye anazidi kupanga njama nzito za kumnasa Daniela. Huko nyumbani kwa Montenegro, Johan na Katerina ni manjonzi tupu kwa kumkosa Daniela kwa ni wote wanamzimikia ile mbaya......

Fuatilia hapa hapa Asili Yetu TZ kwa mwendelezo wa Tamthilia hii ya kusisimua.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.