Diamond baada ya kuzindua perfume yake ya "Chibu Perfume" Waziri aeleza yake mpya ya moyoni.
Siku
chache zimepita toka staa wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake
mpya inayoitwa “Chibu Perfume” na kuonesha kupokelewa kwa nguvu kubwa nchini
Tanzania.
Hatahivyo ubunifu wa wa msanii Diamond umemfikia Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla na kumfanya aandike ujumbe
kuhusu perfume hiyo, huku akimsifia Diamond kwa kufanya vitu vikubwa
pamoja na kukiri kuwa yeye sio shabiki wake isipokuwa anaupenda muziki
wake.
“Sikuwahi
kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema
hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki
wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is
not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and
businessman".


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA