Sherehe za 'Diwali' katika mji wa Delhi India zasababisa hali ya hewa kuchafuka.
Wakaazi wa jiji kuu la India, Delhi wameghathabishwa na kile wamesema
kuwepo ukungu mkubwa uliosababishwa na fataki nyingi zilizorushwa katika
sherehe za Diwali.Mamlaka zilionya uchafuzi wa hewa kutokana na fataki
hizo kutumiwa juu ya kiwango kilichowekwa.
Sherehe za Diwali ni muhimu
sana katika imani ya Kihindi na huadhimisha ushindi wa wema dhidi ya
ubaya.
Urushaji wa fataki huambatana na sherehe za Diwali na wengi huona hii kama ishara ya utajiri.Familia
na kampuni za biashara nchini India hutumia maelfu ya dola kununua
fataki ambazo hurushwa usiku wakati wa sherehe hizo.
Kwa mujibu wa
Shirika la Afya Duniani{WHO} miji 13 kati ya 20 ambayo imechafuliwa
zaidi duniani inapatikana India.
Mkali wa filamu na muziki wa kihindi Shahrukh Khan akiwa na mkali mwenzake maarufu kaka mwadada Kajol. Hapo unakumbuka filamu gani walioicheza wakali hawa?
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA