Bondia Thoma Mashali aaga dunia.
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada
ya kupigwa na watu wasiojulikana, maeneo ya Kimara Jijini Dar es
salaam.
Akithibitisha taarifa hizo, Rais wa Organaizesheni ya ngumi za kulipwa
nchini TPBO Yassin Abdallh “Ostadh” amesema mauti yamemkuta Mashali
baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa na
wasamaria wema maeneo ya Kimara.
Na kwaupande wa Mzee Malifedha Christopher Mashali baba Mzazi wa Thomas Mashali ambaye
ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo huko Kimara jijini
Dar es Salaam amefunguka na kuelezea kilichomkuta mwanaye.
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema Peponi. Amina
Source: EATV
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA