Dalili 10 mbaya uwapo kazini, ukiziona hizi dalili tu jipange.
Na
ili kukuokoa kabla mambo hayajaharibika ni vema ukaanza kuandaa CV zako
mapema. Nimekuwekea hapa dalili 10 za kugundua kama umechokwa ofisini
kwako au na mwajiri wako na wanapanga kukuwashia moto.
- Majukumu Yasiyoeleweka: Mwanzo
wakati unaanza kazi mambo yalikua safi lakini ghafla boss wako anaanza
kukupangia majukumu mengine na ni yale ambayo anajua kabisa huna uwezo
nayo au anakupa majukumu yasiyo na faida yoyote kwake na kwako!
- Haupewi nafasi ya kukutana na Boss wako. Muajiri wako anaanza kukukwepa au hakupi nafasi ya kuongea naye kama mwanzo, na hakupi majukumu yenye faida.
- Boss hapendi kukutana na wewe:
Ni jambo la kushangaza inakuaje mtu aliyekua anakuamini sana ghafla
inatokea hapendi kukutana na wewe iwe ni kwa issue za kiofisi au binafsi
wakati mwanzo alikua anakushirikisha hadi mambo yake binafsi.
- Mipango au ushauri: Mwanzo
ulikua mtu wa kwanza kuombwa ushauri na ulikua unaonekana ni wa maana
sana unaanza kuonekana hauna nguvu wala ushawishi tena. Hauoni ushauri
wako ukifanyiwa kazi kama mwanzo.
- Boss wako anatafuta makosa: Vitu vidogo sana ulivyofanya vinakuzwa na unafokewa sana wakati mwingine unakua hata haujahusika.
- Unatakiwa kuwafundisha wengine: Sio
jambo baya lakini ni la hatari inapotokea boss wako anaanza kukwambia
uanze kuwafundisha watu wengine majukumu yako hasa waliokuwa chini
yako.
- Unajadiliwa sana kwenye vikao:
Muda mwingi Boss wako anazungumza na HR kuhusu utendaji wa wafanyakazi
na milango inakua imefungwa, ukiingia tu wananyamaza mpaka utoke.
- Haualikwi kwenye Vikao muhimu:
Zamani ulikuwa wa kwanza kuambiwa chochote kuhusu vikao vya ofisi
pamoja na maamuzi au mabadiliko yoyote ila sasa haushirikishwi kwa
lolote.
- Unaombwa kuandika majukumu yako mara kwa mara:
Ni jambo la ajabu sana, Boss wako ndiye aliyekupangia majukumu yako
wakati unaajiriwa lakini ghafla anaanza kukwambia umuandikie kazi
unazofanya kila siku. Hapo anza kupanga vitu vyako.
- Unatakiwa kueleza umefanya nini kwenye kampuni: Boss wako anakutaka umuandikie umefanya nini kwenye ofisi yake tangu ulipoajiriwa na unategemea kufanya nini kipya.
Credit: TZA
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA