Utafiti: Kukumbatiwa na yule umpendae wakati wa maumivu, ni zaidi ya dawa ya maumivu.
Kumbatio kutoka kwa mtu umpendaye, linaweza kuwa na nguvu zaidi ya Paracetamol pale unapokuwa na maumivu, kwa mujibu wa utafiti.
Wanasayansi
wamebaini kuwa hisia za ukaribu tunazozipata kupitia mtu anayetushika,
kunaweza kusaidia kupunguza maumivu. Lakini kushikwa na mtu usiyemjua,
kunaweza kusiwe na matokeo yale yake, kwasababu hatuna hisia nao.
Utafiti huo unaonesha nguvu ya ubongo kuzuia hisia za maumivu. Utafiti
huo ulifanywa na wataalam katika chuo kikuu cha Haifa, Israel na
ulihusisha wanawake kadhaa ambao waliwatengenezea maumivu kwa kuwaunguza
na chuma chenye moto kiasi.
Katika jaribio la kwanza, mtu wasiyemjua aliwashika mkono akijaribu
kuwaliwaza kwa maumivu hayo. Kwenye la pili waliwaita waume na wapenzi
wao kukaa karibu nao na kugusanisha ngozi.
Katika jaribio la mwisho, wapenzi wao waliruhusiwa kuwashika mkono
wakati chuma hicho cha moto kikigusishwa kwenye ngozi zao. Wanasayansi
walibaini kuwa mguso wa mtu wasiyemjua pamoja na kuwa na mpendwa wao
karibu hakukuwa na tofauti katika jinsi walivyosikia maumivu.
Lakini pale mtu wanayempenda alipowagusa kwenye ngozi, maumivu yalipungua.
Walibaini pia kuwa kadri mpenzi wa mwanamke alivyoonesha huruma na support kwake wakati wa zoezi hilo, alipata afueni zaidi.
Sorce: Bongo5
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA