TANZANIA WE ARE STILL THE BEST IN AFRICA, NO MATTER WHAT THEY SAY.
![]() |
| Tanzania Yetu |
Japokuwa Tanzania inapambana na mambo mbali mbali ya kisiasa, kiuchumi na uharifu bado Tanzania ni kisiwa cha amani na utulivu. Watu muiishio ughaibuni msidhani Tanzania hakuna amani, La hasha! Kumbukeni maadui hufurahia sana kuiona amani yetu ikiripotiwa kutoweka.
Leo hii dunia nzima ni matumbo joto, vita haziishi, si Afrika si Asia, America wala Ulaya, ni machafuko tuu ya kisiasa, kidini na kiuchumi. Na siku zote wasio na amani wanatamani sote tuwe katika njia moja, njia moja ya majanga tusiyo chekana kamwe.
Nchi zenye choko choko za kisiasa hawalali, chakula ni shida, kila kitu ni tabu tupu! Lakini nashangaa nchi za ughaibuni wanaishikia bango Tanzania, eti oooh Tanzania sasa ni vita, mara mbinguni ya Afrika sasa siyo tena! Hivi kwa habari kama hizi mnajua ni kiasi gani nchi yetu mnavyoitia hasara za kiuchumi?. Haya sawa tunamatatizo kama nchi nyingine, hiyo sii kigezo cha kufanya mambo yazidi kuwa magumu.
Watalii watakujaje Tanzania kama wataendelea kusoma habari katika vyombo vya kimataifa kuihusu Tanzania? Leo hii ukiniuliza mlio wa risasi za kivita siujui, lakini Sudan, Liberia na kwingineko ni kitu cha kawaida na sio kwamba wao wanapenda iwe hivyo bali ni uchochezi wa kisiasa tu.
Jamani tutafute muafaka kwa amani kama uchaguzi wa madiwani jijini Arusha ulivyomalizika kwa amani.
Ni nchi gani duniani isiyokuwa na waandishi wa habari? Ni nchi gani itakayoweza kukuwa kimaendeleo bila waandishi wa habari? Sasa jamani vyombo vya habari vikiandika mazuri tuu na kufumbia macho mabaya tutakuwa tunajenga au tunabomoa? Hata baba asipomkanya mwanae anakuwa hamuandalii maisha mema mbeleni..
Napia waandishi wenzangu tuandike habari za kuijenga Tanzania kwa kiasi kikubwa, hasa katika mitandao ya internet, kumbukeni dunia inatusoma tunayosema na once unachokiandika hakifutiki kamwe katika akili za watu.
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika. Karibu Asili Yetu Tz.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA