Header Ads

Breaking News
recent

WALANG HANGGAN (TAMTHILIA) - EPISODE YA 5&6 DANIEL AUTEKA MOYO WA KATERINA NAKUJIKUTA AKIZAMA KATIKA PENZI ZITO LA KIFICHO.

Daniel, Katerina (kati) na Nathan
Siku ya kuzaliwa ya Katerina inafika, wakiwa katika sherehe hiyo Thomas ambaye ni kaka yake Katerina anawasiri  katika sherehe na kumuanzishia fujo Daniel.


Kwa kifupi sherehe inavurugika na Daniel kuamua kwenda mbali kidogo na makazi yao, sehemu nzuri za miinuko na nyasi za kijani ambapo kando kando yake kunaonekana ufukwe wa bahari. Lakini Daniel akiwa huko na mwenye majonzi, mara Katerina anawasiri katika eneo hilo na kumwagia Daniela lawama nzito kwa kumwalibia sherehe yake, kwani alitegemea mengi kutokea.

Daniela namuomba msamaha lakini Katerina na anazidi kumlaumu Daniela na kusema “umeniharibia sherehe yangu kwa ugomvi, kwani nimekosa vitu vingi vya msingi ambavyo ningevipata” Daniel akiwa bado anashangaa, mara Katerina akagundua kuwa Daniel hakuwa na ile pete inayompagawisha siku zote, hivyo anaamua kumuuliza kama alimpatia msichana mwingine.

Daniel anatabasam na kutoa kitu mfukoni na kukifunua…… woow! Ilikuwa ni ile pete inayompagawisha Katerina siku zote! Katerina anaamuuliza Daniel…. Ni nini hicho? Daniela anatoa ile pete na kumvisha…. Mmmh! Tayari wanakula kiapo kuwa wapenzi katika maisha yao yote…. Ila swala hili bado Katerina anapendekeza liwe siri kwa baba yake mpaka atakapomaliza shule.

Bibi yake Daniel anasanukia mchongo huo na kuamua kuwauliza wakiwa wote wawili, Daniel anaamua kuto mficha bibi yake kuhusu mahusiano yake na Katerina. Bibi yao anawasihi kutofanya mambo ya kikubwa mpaka hapo muda utakapofika……

Kumbuka Tamthilia hii ilianzwa na Marco Montenegro na Emily ambapo Emily aliwekwa jela na mama yake Marco, huku Emily pia akizaa mtoto na kudaiwa kufariki mara tu baada ya kuzaliwa.

Sasa Emily alishatoka Jela na ni tajiri ambaye amepanga kulipiza kisasi kwa familia ya Marco Montenegro. Emily tayari anamtuma mfuasi wake mmoja akiwa kama mfanyakazi katika familia ya Marco ili apeleleze mpango mzima, kwani familia hiyo haikuwepo huko muda mrefu.

Baba yake Katerina anapata safari ya kwenda mji mwingine na kumuagiza pia Daniel kwenda mji wa Manila kumfuatilia Thomas ambaye ni kaka yake Katerina, ili kujua maendeleo ya kampuni aliyodai kuwa anaanzisha.

Kabla Daniel hajaenda Manila, Nathan Montenegro ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Katerina wakati wa utoto ambaye kwa kipindi kirefu hawakuwa wanaonana, alifika ghafla nyumbani kwa kina Katerina na kumuomba waende wote kwa wazazi wake ili kuwasabahi.

Katerina akiwa nyumbani kwa akina Nathan, huku Daniel alianza kumtafuta ikaambiwa kuwa ameondoka na Nathan.
Daniel anaamua kwenda hadi kwa akina Nathan na kuzuiliwa kuingia kwani kulikuwa na walinzi. Kule ndani Nathan anamzuia Katerina kuondoka na kudai anamletea kinywaji. Katerina anaamua kuzunguka zunguka ndani lakini hakuona mtu yeyote, anamua kwenda kibarazani mara anakutana na Daniel ambaye aliamua kuruka ukuta na kuingia huko ndani ya fensi.

Wakiwa bado wamesimama, mara mbwa mkubwa anatokeza na kuwanza kuwafukuza, ila kwa ujasili Daniel anamwambia Katerina “usikimbie jikaze usimame hivo hivo” lakini uzalendo unamshinda Katerina na kuanza kukimbia. Mbwa inamuuma mguu baada ya kuwa ameanguka.

Walinzi wanambeba na kumpeleka ndani, huku Daniel akikatazwa kuingia huku akionyeshewa bastola. Marco Montenegro anampigia simu baba yake Katerina na kumuomba akae kwake ili apone vizuri. Marco anaamua kumpa rifti Daniel kwenda mji wa Manila ambako baba yake Katerina alimuagiza. Lakini huko nyuma fisi anakabidhiwa bucha, yana Katerina anabaki na Nathan….. Je nini kitatokea katika mahusiano ya Daniel na Katerina?

Huko mjini nako Marco Montenegro anamuona Emily kwa macho yake yani live, Je nini kitatokea?
Je nini kitaendelea?  Karibu tena kwa dondoo  nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.