Header Ads

Breaking News
recent

MASKINI “DANIEL CRUZ” AZIDI KUFANYIWA UNYAMA NDANI YA TAMTHILIA YA “WALANG HANGGAN”.


Baada ya Thomas kumfanyia unyama wa kumburuza Daniel Cruz na farasi, hakuridhika kwani sasa Thomas aungana na rafiki zake na kumpa kichapo kibaya japokuwa haikuwa rahisi kwao kwani kama kawaida Daniel Cruz aliwatembezea kichapo, japokuwa wakati huu walimzidi na kumchoma kisu ubavuni na kumtupa mtoni.

Kumbuka chanzo cha Daniel Cruz kupata matatizo yote hayo ni mdogo wake Thomas anayeitwa Katerina ambaye amezama katika penzi la Daniel Cruz. Kwasababu Katerina hakuwepo nyumbani kwa muda mrefu akiwa nyumbani kwa akina Nathan Montenegro sasa aamua kurejea nyumbani kwao ili apate muda mzuri wa kuwa na Daniel Cruz.
Akimuelezea Nanni (bibi yake Daniel Cruz) jinsi Nathan anavyokazana kumtongoza na kumuahidi kumuoa, mara Daniel Cruz alifika kimia kimia na kuyasikia maneno hayo, kitu kilichomsababisha kumwaga machozi na kuamua kwenda porini ambako ndiko Thomas na rafiki zake walimchoma kisu na kumtupa mtoni.

Katerina anashikwa na machale kwa kutomuona Daniel, akiwa na hofu huku akimwaga machozi kama mvua ya elinino ya miaka ya 90 naa, juhudi hizo zinagonga mwamba na kuambulia kwenda kutoa taarifa polisi. Kumbe mpango mzima wa mauwaji ya Daniel Cruz yalipangwa na Nathan Marco Montenegro ambae amekuwa akimgombea Kateria.

Mungu mkubwa Daniel Cruz hakufariki wakati ule alipotupwa mtoni huku akiwa amechomwa kisu ubavuni, alijikongoja hadi kando kando ya bara bara na kupoteza fahamu. Emily adui mkubwa wa familia ya Marco Montenegro wakiwa katika mishe mishe yao wanamkuta Danie Cruz akiwa katika hali mbaya. Emily anawaamrisha watu wake wampakie garini na na kumuwahisha hospitali.

Mungu saidia Daniel Cruz asilimia kubwa anapona akiwa nyumbani kwa Emily. Daniel anadai aondoke na kurudi kwa Thomas, lakini Emiliy anamshauri asirudi mapema bali aandamane nae kwenda katika mji mwingine ambako huko atamtajirisha ili aweze kulipiza kisasi kwa Montenegro na Thomas.

Emily anamuomba Daniel Cruz abadili jina na awe kama kijana wake mkubwa ili Montenegro wasije kumfatilia kwa urahisi. Daniel Cruz bado hajaridhia uamuzi huo, lakini kunakitu kinatokea kinachomfanya akubaliana na wazo la Emily.

Je nini kitaendelea?  Karibu tena kwa dondoo  nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.