Header Ads

Breaking News
recent

HII NDIO JEZI ATAKAYOITUMIA SYDNEY WILHELM GIDABUDAY - (MMAREKANI MWENYE ASILI YA KITANZANIA) KUITANGAZA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA BRONCO INVITATION JUNE 22 CALIFORNIA.

Pichani hapo juu ni jezi ya Tanzania atakayotumia katika mashindano huko Calfornia.
Sydney Wilhelm Gidabuday ni mwanariadha wa kimarekani mwenye asili ya kitanzania na mtoto wa mwanariadha wa kitanzania wa zamani aliyevunja rekodi miaka ya 1994 nchini Marekani ambaye jina lake si geni masikioni mwa watanzania "Wilhelm Gidabuday".

Japokuwa Sydney ni mmarekani mwenye mapenzi na uzalendo wa kuitangaza nchi ya baba yake Gidabuday yani "Tanzania", tayari amekwisha pokea jezi  atakayotinga katika mashindano ya riadha ya BRONCO INVITATION JUNE 22, CALIFORNIA MAREKANI. Jezi ya Tanzania iliyotumwa kutoka Tanzania na wanariadha wa kitanzania yani "Phaustin Baha na Wilhelm Gidabuday, tayari imekwishafika katika mikono ya Sydney huku akiahidi kuitendea haki katika mashindano hayo.

Sydney Wilhelm Gidabuday
MAONI KWA SERIKALI.

Kuwa na uraia wa nchi mbili sio sababu ya kutoipenda Tanzania yetu, bali ni njia muafaka ya kuifungua milango na mianya ya kuleta mafanikio na kulitangaza taifa letu la Tanzania katika nchi mbali mbali duniani.

WITO KWA SERIKALI KUTOKA KWA GIDABUDAY - BABA YAKE "SYDNEY - GIDABUDAY".

"Mimi baba yake, naliomba bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhalalisha SHERIA YA URAIA WA NCHI MBILI ili mtoto wangu "Sydney" aweze kuiwakilisha Tanzania, kwani anauzalendo sana na nchi hii", japokuwa alizaliwa Marekani, huku shule ya msingi akianzia Tanzania".

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.