Header Ads

Breaking News
recent

PICHA: BOMU LA SADIKIWA KULIPUKA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA NA KUJERUHI WENGI, HUKU WENGINE WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA.

Mlipuko wa kishindo ulisikika katika viwanja vya Soweto mjini Arusha, ikiwa ni takribani saa 12 jioni, wakati mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wakiwa katika harakati za kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani unaotarajiwa kufanyika hapo kesho.

Tukio kama hili lilitokea takribani mwezi mmoja uliopita  jijini Arusha lakini kabla uchunguzi ukiwa bado haujatoka, mengine yameibuka upya!!!!!!!

Ripoti kamili haijatoka kutoka jeshi la polisi, lakini inahofiwa kuwa watu wanne wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. Please pray for us!!!

Mheshimiwa Lema akiwahutubia wananchi kabla ya tukio kutokea (Picha na Seria wa Arusha 255)


(PICHANI NI HELICOPTER YA MBOWE WAKATI IKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUTUA SOWETO).

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.