Header Ads

Breaking News
recent

PICHA ZA VIONGOZI WALIOSHIRIKI MBIO ZA KUMBU KUMBU YA "EDWARD MORINGE SOKOINE MINI MARATON 2013" MONDULI - ARUSHA.

 Mhe: Christopher Olesendeka - Mbunge wa Simanjiro akishiriki mbio za Mini Marathon ya kumbu kumbu ya hayati "Edward Moringe Sokoine 2013" Wilayani Monduli siku ya jana.

 Mhe: Godbless Lema - mbunge wa Arusha Mjini aliyevalia ngwanda la kaki na namba kifuani akiwa katika mstari wa kuandikishwa baada ya kumaliza mbio kilometa 2 za Mini Marathon ya kumbu kumbu ya hayati "Edward Moringe Sokoine 2013" Wilayani Monduli siku ya jana. Mbele yake ni Seria mwenye blog ya Arusha 255 akiwa nae kashiriki mbio hizo.

Mhe: Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara akiwahutubia mamia ya watu walio hudhuria siku ya kumbu kumbu ya kutimiza miaka 29 ya hayati waziri mkuu "Edward Moringe Sokoine" huko Monduli.

Waziri Mkangara aliwaomba wananchi kuikumbuka siku aliyofariki Edward Sokoine 12/4/1984 pamoja na mema aliyowatendea wananchi wake.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara (wakwanza kushoto), akifuatia Mbunge wa Monduli Edward Lowasa (Aliyevaa nguo ya blue), katikati ni Binti wa hayati Edward Sokoine - Mbunge wa CCM viti maalum "Namelok Sokoine", akifuatiwa na Mbunge wa Simanjiro - Christppher Olesendeka, wakishuhudia tukio lambio likianza rasmi.

Viongozi na wanafamilia wakishuhudia matukio ya michezo yaliyokuwa yakiendelea.

Waziri waHabari Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara akiwa na wabunge wakati wa mbio za Mini Marathon ya kumbu kumbu ya hayati "Edward Moringe Sokoine 2013" Wilayani Monduli siku ya jana.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.