MCHEZAJI WA ZAMBIA CHRISTOPHER KATONGO ANYAKUA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA BBC 2012.
Chris Katongo baada ya kupokea tuzo ya mwanasoka bora wa BBC
Christopher Katongo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa BBC mwaka wa 2012.
Orodha ya washindani hao ilitengazwa na wataalamu wa soka Afrika, ambao wamezingatia umahiri wa mchezaji, uwezo wa kiufundi na ushirikiano na wachezaji wengine.
Na idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku asilimia 40 kati yao wakimchagua Katongo, ambaye anachezea timu ya China Henan Construction.
Katongo aandikisha rekodi mpya
Huku wachezaji wote walioorodheshwa katika kinyang'anyiro hicho walikuwa na mwaka mzuri, wanne kati yao walikuwa wameshinda medali mbali mbali, ni Katongo pekee ambaye mafanikio yake yamezingatiwa na mashabiki wa mpira Afrika.
Chris Katongo akipokea tuzo hiyo kutoka kwa waziri
Alifunga magoli matatu katika fainali iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon na baadaye kufunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti na kuisadia Zambia kunyakuwa kombe hilo.
Zambia iliishindi Ivory Coast kwa 8-7 katika fainali hiyo baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu baada ya muda wa kawaida na muda wa ziada mjini Libreville.
Katongo afufua matumaini ya Zambia kuelekea Brazil
Chris Katongo akishika tuzo aliyoshinda
Miezi saba baada ya kuongoza Zambia kushinda kombe hilo, Katongo vile vile amekuwa nyota wa timu yake ya taifa wakati wa michuano ya kufuzu kwa fainali za mwaka ujao,wakati alifunga goli la pekee dhidi ya Uganda.
Bao hilo liliibuka kuwa bao muhimu sana kwa Zambia kwa kuwa ilipoteza mechi iliyofuatia kwa bao moja kwa bila, lakini ikafuzu kwa fainali za mwaka 2013 zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini baada ya kushinda kwa magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.
Mikakati ya kufuzu kwa kombe la Dunia
Na zaidi ya hayo yote, Katongo amechangua pakubwa harakati za kufufua matumaini ya Zambia ya kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2014.
Naodha wa Zambia Chris Katongo
Wiki moja baada ya mechi hiyo Zambia ilichuana na Ghana na Katongo kwa mara nyingine ndiye aliyefunga bao la ushindi na hivyo kuimarisha matumaini yao ya kufuzu.
Source: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA