Header Ads

Breaking News
recent

KOCHA WA HARAMBEE STARS YA KENYA, AJIHUZULU.


Henri Mitchel
Aliyekuwa kocha wa Kenya
Kocha wa Harambee Stars Henri Michel amejiuzulu miezi minne tu baada ya kusaini mkataba na shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya FKF.

Kocha huyo kutoka Ufaransa, amekuwa kwenye mgomo baridi baada ya FKF kutomlipa mshahara wake wote.
Michel hulipwa shillingi milioni nne na manaibu wake wawili nao hupokea mshahara wa milioni moja unusu.
Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Ubalozi wa Ufaransa mjini Nairobi kocha huyo anarejea nyumbani hii leo.

Hata hivyo barua hiyo inaashirikia kuwa kocha huyo alijiuzulu tarehe kumi mwezi huu lakini tangazo hilo limetolewa leo tarehe 17 Desemba.
Michel alikataa kuongoza Harambee Stars wakati wa michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, akiitaja mashindano hayo kama mashindano yasiyokuwa na maana yoyote.

Henri Mitchel
Aliyekuwa kocha wa Kenya Henri Mitchel
Kocha huyo alisema jukumu lake kuu ni kuhakikisha Kenya imejianda vyema kwa michuano ya kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani.
Awali rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya Sam Nyamweya alikariri kuwa kocha huyo alikuwa na jukumu la kuandaa Harambee Stars kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka wa 2014.

Source: BBC

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.