FILAMU YA KUMSHUKURU RAIS JAKAYA KIKWETE.
SHUJAA ZAWADI KWA Mh.KIKWETE
Amani ni mmoja wa vijana aliyeguswa na kitendo cha Rais
JAKAYA
MRISHO KIKWETE cha kuamua kupima VVU hadharani .Naye kuanzia
hapo
alijiwekea utaratibu wa kufanya hivyo kila baada ya miezi
mitatu, na
kwa bahati nzuri alikuja kufanya kazi katika shirika
linaloshugulika
na na kupima VVU na Ushauri nasaha. Siku moja alikutana na
binti mzuri
Fransisca akiwa katika mazingira ya kujiuza (changudoa).
Alimuona ni
mzuri sana akampenda, na akataka kujua zaidi .Hadithi ya
maisha ya
yule msichana ndio yanamfanya amani awe na imani zaidi
.Lakini jambo
moja linatatiza kati yao je yule msichana ni salama? hakuna
kinachoweza kufumbua fumbo hili zaidi ya kwenda kupima kitu
ambacho
Francisca hakuwa tayari kutokana na idadi ya wanaume
aliotembea nao.
Ugumu wa jambo hilo haumkatishi tamaa amani, hatimaye
anafanikiwa
kuokoa maisha ya msichana huyo. Na kutimiza ndoto zake za
kuwa shujaa
kama Raisi Jakaya Kikwete.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA