Header Ads

Breaking News
recent

DOCTOR WA UPASUAJI MWENYE UMRI WA MIAKA SABA AWASHANGAZA WATU.

Akrit Jaswal ni kijana mdogo wa kihindi aliyeitwa kijana mtanashati katika dunia nzima, kwa maajabu aliyonayo. Kijana huyu ana IQ 146 na anahesabika kuwa ndiyekijana mtanashati katika nchi ya India yenye mabilioni ya watu.

Akirt alianza kufahamika rasmi mwaka 2000 alipoanza kujihusisha na matibabu akiwa nyumbani kwao, wakati huo akiwa na umri wa miaka saba. Kwa mara ya kwanza alimfanyia upasuaji wa vidole msichana mmoja mwenye umri wa miaka nane ambaye alikuwa ameungua na moto katika vidole vyake na kusababisha vidole hivyo kuungana na kushindwa kufanya kazi.

Kwa kuwa msichana huyo alikuwa hawezi kumudu gharama za kwenda hospitali kubwa kufanyiwa upasuaji wa vidole vyake, lakini mvulana huyu Akrit ambaye hakuwa na elimu yoyote ya udaktari aliweza kumfanyia upasuaji msichana huyo, nyumbani kwao kwa wazazi wake na kuweza kufanikisha zoezi hilo na hatimae msichana yule aliweza kupona na kutumia mkono wake tena.

Kijana huyo alielekeza akili yake yote katika madawa na alipofikia umri wa miaka 12 alikuwa katika hatihati ya miongoni ya watu waliyogundua dawa ya kutibu ugonjwa wa Kansa. Sasa yuko katika chuo kikuu cha Kandigarh akichukua digree yake ya sayansi huku akiwa ndiye mwanafunzi mdogo kabisa kukubalika kujiunga na chuo kikuu nchini India.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.