Header Ads

Breaking News
recent

MTU MMOJA ACHOMA VISU WATOTO 22 WA SHULE YA MSINGI HUKO NCHINI CHINA.

Kijana mmoja amewachoma visu wanafunzi 22 wa shule ya msingi na mtu mzima mmoja huko nchini China, majira ya asubuhi siku ya Ijumaa wakati watoto hao wakiingia shuleni.

Kijana hyuo mwenye umri wa miaka 36 alifanaya tukio hilo ikiwa ni kabla ya saa mbli za asubuhi, ambapo baada ya kufanya kitendo hicho alikamatwa na polisi na kuwekwa rumande.

Hatahivyo watoto wote waliochomwa visu hakuna aliyefariki, bali wakiwa katika matibabu, 9 wamekwisha ruhusiwa kurejea makwao, huku wawili wakiwa katika hali mbaya kwasababu ya kudhurika kwa kiasi kikubwa, wengine bado wanapatiwa matibabu hospitalini.

 Tukio hili limeambatana na lile lililotoke hivi karibuni nchini marekani ambapo takribani watoto wadogo wa shule ya msingi nao waliuwawa kwa risasi na raia mmoja wa nchi hiyo.Pia tukio kama hilo la kuuwawa wanafunzi lilitoke hivi karibuni nchini Nigeria ambapo wao walikuwa ni wanafunzi wa chuo kikuu.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.