CHADEMA MKOA WA ARUSHA YAPATA VYOMBO VYA MUZIKI KWA AJILI YA MIKUTANO
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema
akiwa anawashukuru wanachini na wadau ambao walifanikisha ununuzi wa vyombo vya
chama mkoa wa arusha wakati walipokuwa
wameudhuria kwenye eventya M4C-JOIN THE CHAIN iliyofanyika katika ukumbi wa
hotel ya snowcrest jijini Arusha.
Lema akiwa na baadhi ya wanachama ambao ni wadau wakubwa wa
chama cha demokrasia na maendeleo chadema ambapo alisema kuwa wadau hawa
wanatarajia kuingia katika majimbo mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya
kuwaletea watanzania ukombozi.
Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa
arusha Amani Golugwa.
Kwaupande wake Katibu wa mkoa Chadema Amani Golugwa
aliwashukuru sana wadau wote ambao wameuthuria na kushiriki katika shughuli hii
ya kuchangia vyombo pamoja na kuchangia gari lakubebea vyombo na alibainisha
kuwa wakati huu ni wa mabadiliko wanafanya kazi kwakusonga mbele na
hawatakubali kurudishwa nyumba huku akibainishakuwa wakati huu sio wakuulizana
nani mwizi bali ni wakati wa kukamata mwizi nakufanya kazi tu
Alisema kuwa swala la mabadililiko ni mpango wa mungu hivyo
hakuna mtu yeyote ambaye anawezakuzuia mipango wa mungu aku akisema kuwa
wanajua itachukuwa muda lakini lazima mabadiliko yatatokea tu.
Aliseongeza kuwa kwakipindi hichi wameamua kuanzisha M4C
JOIN THE CHAIN hiii ikiwa ni njia ya
kuleta mabaidiliko huku akisema kuwa wanataka wanyakuwe majimbo yote ya mkoa wa Arusha
"unajua tunataka tunyakuwe majimbo yote ya mkoa wa
arusha nakwanza kabla ya kuyachukuwa tunataka tuanze kuwaonyesha wananchi
katika baadhi ya halmashauri tulizo zichukuwa ambapo alisema kuwa wao kama chadema mkoa wa Arusha wanamiliki halmashauri mbili
ambayo ni halmashauri ya meru pamoja na karatu ambapo alisema hizi ndo anataka
ziwe za mfano katika kuleta maendeleo.
Alifafanua kuwa vyombo vya mziki vilivyonunuliwa (pa
system)viligharimu kiasi chashilingi
milioni 14 na laki sita ,huku
kiasi cha shilingi milini 27 zikiwa ni ahadi kwaajili ya gari na keshi ikiwa ni
shilingi milioni moja.
Source: Libeneke La Kaskazini


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA